Saturday, April 30, 2022

Latra yatangaza bei Mpya za Mabasi 2022

 


Mamlaka ya udhibiti wa usafiri nchi kavu (LATRA) imetangaza bei mpya za nauli za mabasi na daladala nchini ambazo zitaanza kutumika baada ya siku 14 kuanzia leo.


Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Gilliard Ngewe amesema nauli za daladala kuanzia KM 0-10 nauli itakuwa Tsh. 500 kutoka Tsh. 400 na  KM 11-15 nauli itakuwa Tsh. 550 kutoka Tsh. 450 na bei ya mwisho ya daladala kwa KM 36 hadi 40 itakuwa Tsh. 1100 kwa daladala tu.


Kwa upande wa nauli za mabasi yaendayo mikoani zimepanda kwa daraja la kawaida ni Tsh. 41.29 kwa KM moja kutoka Tsh. 36.89 huku daraja la kati likipanda kwa shilingi 56.88 kutoka Tsh. 53.22.


Nauli kwa wanafunzi imebakia kuwa Tsh. 200 kwa daladala...swipe kuona bei zote

0 comments:

Post a Comment