Thursday, August 25, 2016

serikali kuinua sekta ya afya

Imeelezwa kuwa Vifo vitokanavyo na Uzazi kwa kinamama bado ni changamoto kubwa Sekta ya Huduma ya Afya

MDR baby_0
Imeelezwa kuwa Vifo vitokanavyo na Uzazi kwa kinamama bado ni changamoto kubwa katika Sekta ya Huduma ya Afya kutokana na maendeleo madogo ya Upunguzaji vifo hivyo vinavyotokana na Ujauzito hali ambayo pia inadaiwa kuchangiwa na  baadhi ya wahudumu wa wa afya kwa kutoa usimamizi na uangalizi mdogo kwa wamama wajawazito pindi wanapofika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuhudumiwa.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amsema wamama wengi hupoteza maisha wakiwa wanajifungua  ambapo amedai  kuwa mpaka sasa vifo 432 vya wamama wajawazito hutokea kwa kila vizazi hai laki moja hapa nchini hali ambayo imekuwa tishio na janga kwa Taifa na kusisitiza juhudi za haraka zichukuliwe ili kutokomeza changamoto hiyo.
Aidha Waziri Ummy Mwalimu pia amesema kuwa Wizara ya Afya inajipanga kutokomeza Ugonjwa wa Malaria ambao unadaiwa kkuongezeka kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 18 hali ambayo pia inadaiwa kuleta hatari kwa wananchi huku wakisisitizwa kufata kanuni za afya za kuzuia malaria ikiwemo kutumia vyandarua vyenye dawa pamoja na kufukia mazalia ya mbu karibu na mazingira yaliyowazunguka ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa huo.
Vilevile Waziri Ummy amewataka watoa huduma za afya katika kila kituo cha afya nchini kuendelea kutoa matibabu bure kwa wamama wajawazito,watoto walio chini ya Umri wa miaka mitano pamoja na Wazee wasiojiweza huku pia akitangaza kufuta Gharama za matibabu kwa watoto waliochini ya miaka 18waliobakwa na kulawitiwa pindi wanapokimbizwa Hospitalini kupata huduma.
Tangu kuingia madarakani Mh.john Pombe Magufuli,sekta ya afya imeweza kuinuka kwa kiasi kikubwa sana ukilinganisha na hapo mwanzo.Katika utekelezaji wa ahadi zake Mheshimiwa Dr.john Magufuri amesha sambaza vitanda katika hospitali nyingi hapa nchini na kuboresha miundombinu kuwa rafiki kwa wagonjwa na wauguzi

0 comments:

Post a Comment