YOUR WELCOME By ADMIN JERRY KIHUNDO

Let me take this golden chance to welcome everyone around the World,remember that your opinions are very important to us - tanzaniabeautiful.blogspot.com.

M0UNTAIN KILIMANJARO

Kilimanjaro is one of the world's most accessible high summits, a beacon for visitors from around the world. Most climbers reach the crater rim with little more than a walking stick, proper clothing and determination.

MIKUMI

Mikumi National Park abuts the northern border of Africa's biggest game reserve - the Selous – and is transected by the surfaced road between Dar es Salaam and Iringa. It is thus the most accessible part of a 75,000 square kilometre (47,000 square mile)

LET US JOIN TO STOP THIS

No child should be working. Every child has the right to a good education, the right to play and the right to enjoy its childhood. Child labour means that poverty continues to exist. Eradicating child labour means development and better opportunities for everyone.

WE ALL FRIENDS

Everyone is equal in the eyes of God. However people blacks and whites are treated differently in other contries but TANZANIA love and hospitality is our tradition

Thursday, October 13, 2016

TANZIA: Aliyewahi kuwa Meya wa Dar, Dr. Didas Massaburi afariki, Rais atuma Salamu za rambirambi


Aliyewahi kuwa Meya wa Dar na Mbunge wa Afrika Mashariki, ndg Didas Masaburi amefariki dunia usiku huu hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.

image.jpeg 

UPDATE:

Rais Magufuli atuma Salamu za Rambirambi familia ya Meya Mstaafu wa Jiji la Dar es Salaam Marehemu Didas Masaburi.

14725547_1008276552616652_4879696274680473689_n.png

Monday, October 10, 2016

TANZANIA KUJENGWA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MAGARI

Gari la kwanza Tanzania kutengenezwa Desemba, 2016

Kampuni ya Simba Motors imesema ina mpango wa kujenga kiwanda cha kuunganisha magari aina ya pick-up ambacho kitaanza kuzalisha magari kabla ya Desemba 30, mwaka huu.



Gari la kwanza Tanzania kutengenezwa Desemba, 2016 MONDAY , 10TH OCT , 2016 Kampuni ya Simba Motors imesema ina mpango wa kujenga kiwanda cha kuunganisha magari aina ya pick-up ambacho kitaanza kuzalisha magari kabla ya Desemba 30, mwaka huu. Ahadi hiyo imetolewa leo mchana (Jumatatu, Oktoba 10, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Jitesh Ladwa mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam. “Tumeamua kuunda magari aina ya pick-up kwa sababu ya mahitaji makubwa yaliyopo nchini. Takwimu zinaonyesha kuwa, kwa mwaka Tanzania inanunua magari ya aina hii zaidi ya 4,000. Katika nchi za SADC mahitaji ni pick-up 35,000 kwa mwaka. Tutaanza na mtaji wa dola za Marekani milioni 200 na tumeomba ekari 200 katika eneo la EPZ,” amesema. “Eneo la kiwanda cha kuunganisha magari peke yake linahitaji ekari 50, kwa hiyo tukiweka na yadi za kupaki magari, eneo la viwanda vingine, eneo la kushusha na kupakia makontena yatakayokuwa yakisafirishwa kwenda nchi jirani, ni lazima tutahitaji eneo kubwa zaidi,” amesisitiza. Amesema mradi huo wa majaribio, utaanza kwa kutengeneza magari 20 kila mwezi na kwamba kazi ya utengenezaji magari itaongezeka na kufikia 1,000 na baadaye 5,000 kwa mwaka. “Tunataraji gari la kwanza litazinduliwa kabla ya Krismasi, mwaka huu,” amesema. Bw. Ladwa amesema uundaji wa magari hayo aina ya Foton-Tunland utafanyika kwa ubia baina ya kampuni yao, SUMA-JKT na kampuni Foton International ya China kwa kutumia teknolojia ya Kichina na kwamba magari hayo yanayotumia 4-Wheel Drive, yana uwezo wa kupita kwenye barabara za aina zote. Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni hiyo, Bw. Aatish Ladwa, amesema mradi utakapoanza, mbali ya kutoa ajira kwa Watanzania, utawezesha pia kujengwa kwa viwanda vingine vitakavyotengeneza matairi ya magari, vioo, taa, bumpers, viti na filters. “Tunataraji kujenga uwezo wa wahandisi wazawa, uhamishaji wa ujuzi kwa mafundi wa Kitanzania (technology transfer), kupunguza bei kwa mlaji wa mwisho, kupunguza gharama za uzalishaji, kutekeleza amza ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa ni nchi ya viwanda, kuongeza ajira kwa wanajeshi, na kuwezesha upatikanaji wa vipuri vya magari kwa urahisi na kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.” “Kiwanda kitaajiri wafanyakazi 1,500 kwa kuanzia ambao watakuwemo mafundi na watoa huduma mbalimbali, lakini katika kipindi cha miaka mitatu hadi mitano, tunataraji kuongeza wafanyakazi wengine 5,000 wakati uzalishaji ukiwa umepamba moto,” amesema. Kwa upande wake, akizungumza mara baada ya kulikagua gari la mfano aina ya Foton-Tunland, Waziri Mkuu amesema anawakaribisha kwenye uwekezaji huo hasa ikizingatiwa kuwa magari hayo yana uwezo wa kupita kwenye maeneo ya vijijini ambako barabara zake siyo nzuri. “Ofisi za Serikali zinayahitaji zaidi haya magari, hospitali zetu za wilayani nazo pia zinayahitaji haya magari ili yaweze kutoa huduma za chanjo kwa watoto, huduma za UKIMWI, kampeni za kupambana na malaria, na huduma kwa mama wajawazito huko vijijini,” amesema.

CUF WAIBUKA KIDEDEA MAHAKAMA KUU



Mahakama kuu Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo tarehe 10/10/2016 imetoa ushindi kwa Chama cha Wananchi (CUF) kwa kutoa kibali cha kisheria kwa chama kuwasilisha ndani ya siku 14, kesi ya kuiomba mahakama kutengua maamuzi batili ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini, kwani maamuzi hayo batili yametengua maamuzi halali ya vikao halali vya chama. Mawakili wa CUF wakiongozwa na Mhe. Juma Nassor, Mhe. Daimu na Mhe. Hashim Mziray wamewaahidi wanachama wa CUF nchi nzima kwamba wataifungua kesi husika ndani ya wiki hii. Kwa kawaida, uamuzi wa leo wa Jaji Munisi huweza kufanywa upande mmoja (EXPARTE) kama ilivyofanyika.

Thursday, October 6, 2016

volcanic sign found at Kagera


Leo October 6 2016 imeripotiwa habari ikitokea eneo la Katarabuga, kata ya Bwanjai wilaya ya Misenyi Kagera ambapo wananchi wa bonde la Katarabuga wamepatwa na taharuki baada ya kuibuka moto ardhini wakidhani volcano. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Prof. Abdulkarim Mruma  amesema moto huo ni wa kawaida tu hivyo wananchi wasiwe na taharuki yoyote.
Prof. Mruma  akitoa ufafanuzi juu ya uvumi huo amesema moto huo ni wa kawaida na kwamba unatokea kwenye ardhi ambayo ina uozo wa majani mengi na yale majani yakiungua yanatoa kitu kama hicho. Prof. Mruma  ameongeza kuwa moto wa namna hii mara nyingi unatokea kwenye makaa ya mawe mtu anapita anaangusha moto mkaa unalipuka panaanza kuungua na ardhi inachubukachubuka kama ilivyotokea kwenye ebneo hilo.
SONY DSC
07 04
SONY DSC
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)

TAARIFA RASMI YA KUPIGWA VIBAYA KWA MWANAFUNZI WA MBEYA DAY

TAARIFA RASMI YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KUHUSU TUKIO LA KUPIGWA MWANAFUNZI, MKOANI MBEYA.
Image may contain: one or more people

Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A Mbeya day sec school anayeishi Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzoni. Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga kama inavyoonekana kwenye video.
Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl Esther Harembo wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali. Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo.
Imetolewa na:
MWIGULU Nchemba,
Waziri wa Mambo ya Ndani.