Thursday, October 6, 2016

TAARIFA RASMI YA KUPIGWA VIBAYA KWA MWANAFUNZI WA MBEYA DAY

TAARIFA RASMI YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KUHUSU TUKIO LA KUPIGWA MWANAFUNZI, MKOANI MBEYA.
Image may contain: one or more people

Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A Mbeya day sec school anayeishi Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzoni. Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga kama inavyoonekana kwenye video.
Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl Esther Harembo wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali. Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo.
Imetolewa na:
MWIGULU Nchemba,
Waziri wa Mambo ya Ndani.

0 comments:

Post a Comment