Monday, October 10, 2016

CUF WAIBUKA KIDEDEA MAHAKAMA KUU



Mahakama kuu Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo tarehe 10/10/2016 imetoa ushindi kwa Chama cha Wananchi (CUF) kwa kutoa kibali cha kisheria kwa chama kuwasilisha ndani ya siku 14, kesi ya kuiomba mahakama kutengua maamuzi batili ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini, kwani maamuzi hayo batili yametengua maamuzi halali ya vikao halali vya chama. Mawakili wa CUF wakiongozwa na Mhe. Juma Nassor, Mhe. Daimu na Mhe. Hashim Mziray wamewaahidi wanachama wa CUF nchi nzima kwamba wataifungua kesi husika ndani ya wiki hii. Kwa kawaida, uamuzi wa leo wa Jaji Munisi huweza kufanywa upande mmoja (EXPARTE) kama ilivyofanyika.

0 comments:

Post a Comment