YOUR WELCOME By ADMIN JERRY KIHUNDO

Let me take this golden chance to welcome everyone around the World,remember that your opinions are very important to us - tanzaniabeautiful.blogspot.com.

M0UNTAIN KILIMANJARO

Kilimanjaro is one of the world's most accessible high summits, a beacon for visitors from around the world. Most climbers reach the crater rim with little more than a walking stick, proper clothing and determination.

MIKUMI

Mikumi National Park abuts the northern border of Africa's biggest game reserve - the Selous – and is transected by the surfaced road between Dar es Salaam and Iringa. It is thus the most accessible part of a 75,000 square kilometre (47,000 square mile)

LET US JOIN TO STOP THIS

No child should be working. Every child has the right to a good education, the right to play and the right to enjoy its childhood. Child labour means that poverty continues to exist. Eradicating child labour means development and better opportunities for everyone.

WE ALL FRIENDS

Everyone is equal in the eyes of God. However people blacks and whites are treated differently in other contries but TANZANIA love and hospitality is our tradition

Wednesday, February 15, 2017

Agness Masogange ndani kwa madawa ya kulevya.....stori nzima hii hapa

TAARIFA zilizotufikia, zinaeleza kwamba Video Queen maarufu Tanzania, Agness Gerald almaarufu "Masogange", anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central) akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.

IMG_3342.JPG 

Masogange alikamatwa na Polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba mpaka sasa bado anashikiliwa central.

Mwanadada huyo anaingia kwenye orodha ya wasanii wengine na watu maarufu nchini, walioshikiliwa na wanaoendelea kushikiliwa wakihusishhwa na sakata la matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya, katika vita kali inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Taarifa zaidi kuhusu kukamatwa kwa Masogange zitafuatia...

> Ikumbukwe kuwa tuhuma za Mlimbwende huyu kuhusika na mtandao wa baishara za Dawa za Kulevya zilishawahi kujadiliwa katika uzi huu => Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

sorce jamii forum

Thursday, February 9, 2017

wema atinga mahakamani,stori nzima hii hapa

Wema asomewa mashtaka, aachiwa kwa dhamana

THURSDAY , 9TH FEB , 2017
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu na wenzake wawili wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi ya leo na kusomewa mashitaka matatu yanayohsiana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.Image may contain: one or more people and sunglasses



Wema Sepetu akiwa mahakamani leo
Akisomewa mashtaka na wakili wa serikali Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba imeelezwa kuwa msanii huyo alikutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya aina ya bangi kiasi cha gramu 1.08.
Akisoma Shtaka hilo linalowakabili watuhumiwa wote watatu, mbele ya Hakimu Huruma Shaidi wa Mahakama hiyo, Wakili wa Serikali Mtalemwa Kisenyi ameiambia mahakama hiyo kuwa siku ya tarehe 4 mwezi wa pili mwaka 2017 katika eneo la Kunduchi Ununio Jijini Dar es Salaam watuhumiwa hao watatu akiwemo Wema Sepetu walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa ya kulevya kifungu cha 17 (1) (a) cha makosa hayo.
Washtakiwa wote wamekana shitaka hilo, kisha kuachiwa kwa dhamana ya shilingi Milioni 5 na kuwa na wadhamini wawili kila mmoja huku uchunguzi ukiendelea ambapo kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 22 mwezi wa pili mwaka 2017.
Kesi hiyo iko chini ya Hakimu Huruma Shaidi, na mwendesha mashitaka Mtalemwa Kishenyi

Manji akasilishwa na kuchafuliwa jina,story na video yote hii hapa

Leo hii, muda mfupi ujao, Yusuf Manji ataongea na Wanahabari. Haijajulikana anataka kuongelea nini.
Nitatoa Updates hapa hapa JF.

Stay tuned.

=======

Manji: Nimesikia wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa.

Manji: Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu Mzee Manji(Manji ni jina kubwa duniani) na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Club Kubwa Barani Afrika Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa.


a2f05f99-ff53-4c1a-aac0-a83f597803fa.jpg

Manji: Na chaguzi zilizopita mimi nilichukua fomu peke yangu ya kugombea Yanga hivyo naheshimika.

Manji: Huwezi kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kutuo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri.

Manji: Na Katiba inasema kila mtu ana haki yake, ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima.

Manji: Ukinishutumu mimi ni mpumbavu tu wewe.

Manji:
 Kama unataka mimi nikusaidie kutaja wauzaji ni kuniweka kwenye hatari. Ulitakiwa unifuate kisirisiri kuniuliza ili kunisaidie.

Manji:
 Mimi nitaenda Kituo cha Polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa.

Manji:
 Kifungu cha 66 katika katiba kinaeleze haki zangu na kifungu 32 pia. Vinanilinda. Kunitaja kwenye list ya wauzamadawa ya kulevya wakati sihusiki ni kuvunjia haki zangu.


Manji: Nataka nimshitaki Mahakamani na vyombo vyote vilivyoandika kunituhumu na madawa.

Manji: 
Kesho naenda Polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki yangu. Huwezi kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.

Manji:
 Wapo watu kwenye mtandao wameanza kuandika vitu, Alichofanya Mkuu wa Mkoa ni kosa siwezi kukubali.

Manji:
 Na Wanayanga kama mnaona mimi sifai na kama hamna imani na mimi hata kesho naondoka Yanga. Siwezi kuchafua Club kubwa.

Manji: 
Kwanini RC Makonda hajamuita Askofu Pengo au Mashehe wamsaidie? Manji ndo umeona wa kukusaidia?

Manji:
 Hiwezi kuniita mimi kama Mbwa njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho utanikuta mimi kwenye gazeti na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki.

Manji: 
Zipo njia za kushughulikia vitu, Tukienda Comoro tunaenda na bendera ya Tanzania. Leo umenichafua, kesho tukienda Comoro tutaonekana watanzania ni wauza madawa.

Manji: Kama unataka msaada wa kukusaidia kukutajia majina ya wauza dawa za kulevya omba msaada sio unaagiza msaada, Unaniita na watu 65 nikae kwenye foleni, watu 65 watamaliza saa ngapi? Huyu si anataka nitoke Saa tano usiku? Sina kazi nyingine za kifanya?

Manji: 
Yupo mzee mmoja na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamdai shilingi moja. Unanihusisha mimi jina langu nililoachiwa na baba la Manji kwenye huu upumbavu halafu unathubutu kiniita kaka yako?

Manji: 
Hii itanifanya nishindwe kwenda Comoro na Klabu ya Yanga sababu Wanacomoro watasema nimepeleka madawa. Wananichafua sana.

Manji: 
Hivi ni vita na nawaunga mkono na wanahitaji msaada wa haraka na kama wana shutuma au ushahidi au wanataka huo msaada wanieleze. Kama vita kwanini isiwe leo wasubiri Ijumaa. Mimi naenda kesho.

Manji: 
Kesho nyie watu wa magazeti na habari msitoe habari kwa upande mmoja.

Manji: 
Ambao hawatabalance habari. Cybercrime inasema ukiweka habari ya uongo unafungwa. "Ambaye ataandika makonda manji dawa za kulevya" kesho namshitaki.

Manji: 
Wakina Amina Chifupa walitaja majina, yalienda wapi? Hii jitihada hakuna mtu anakataa. Hata unayemchunguza humtaji kwenye vyombo vya habari. Hata TAKUKURU hawawataji wanaowachunguza. Mimi siwezi kwenda kutaja mshahara wa mfanyakazi wangu kwenye radio, uwezo ninao lakini nitakiwa namvunjia heshima.

Manji: 
Mimi nipo tayari kupimwa kama natumia madawa na kupekuliwa nyumbani kwangu na Makonda naye apimwe kama anatumia madawa na wampekue pia nyumbani kwake.

Manji: 
Ninayo Mengi ya kusema, lakini sitaki kuchanganya vitu viwili kwenye mkutano mmoja. Kesho au keshokutwa nitafanya mkutano na nitazungumzia kuanzia PSPF, Coco Beach nk. Leo nakaa kwenye point moja tu ya madawa.

Manji: 
Huyu Mkuu wa Mkoa kwanza nilikuwa simjui, ila kunasehemu nimewahi gongana naye Oysterbay na siku nyingine nilienda kuonanana naye ofisini kwake kama Diwani wa Mbagala Kuu kumuomba afikishe ombi langu kwa rais ili Mkuu wa majeshi atakayekuja ahamishe kambi ya jeshi kutoka Mbagala na kupelekwa nje ya mji (Ile kambi ambayo mabomu yalilipuka).

Kama Diwani siwezi kumuandikia rais.

Wednesday, February 8, 2017

RC Makonda atumbua jipu,Nimajina Mapya ya ya wanao jihusisha na Dawa za kulevya jijini Dar es salaam


Kumekucha!!Ni siku nyingine tena,Mkuu wa Mkoa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dsm,ndugu Paul Makonda ataongea leo na waandishi wa habari kuhusu muendelezo wa vita ya madawa ya kulevya ktk jiji la Dsm.

Mkuu wa Mkoa atakuwa mubashara Azam Tv mara ifikapo saa 05:00 asubuhi leo hii.

Tetesi ni kuwa,mkutano huo unaweza kuwa ni kujibu tuhuma za kuwa anawakabili "dagaa" na wakati "mapapa" wa biashara hiyo wapo.Na majibu ya mkuu wa mkoa yatakuwa ni kuwataja hao mapapa na kuelezea hatua zitakazochukuliwa...

Tega usikie....(Stay Tuned)

=======
UPDATE:
=======

Ameanza kwa Kumshukuru Rais wa Jamuhuri.

Paul Makonda asema anataka wauzaji wa dawa za kulevya wajulikane hadharani na hakuna sababu ya kuficha.

Paul Makonda asema vita vya dawa za kulevya vilianza muda mrefu kwa kufutilia hali ilivyo mitaani.

'Kuna watu nilitaka nikutane nao polisi, kuna tofauti kati ya kukamatwa na kuitwa, unapoitwa unapewa nafasi ya kusikilizwa'-RC Makonda


'Kampeni hii dawa ya dawa za kulevya si ya kufanyika kimyakimya tunataka hata watoto wadogo wajue dawa hizi ni hatari kwa afya'-RC Makonda

'Asante kwa watu kama TID, nawapongeza kwa kukiri na kusema kuwa wanatambua namna walivyoingia na kuomba serikali kuwasaidia'-RC Makonda

'Tumemaliza awamu ya kwanza vita ya dawa za kulevya, sasa hii ni awamu ya pili ambayo itakuwa si nyepesi itakuwa na mawimbi mengi-Makonda

'Awamu ya 2 ya vita ya dawa za kulevya tunaianza leo na tunaianza tukiwa tumekamilika, nimekuwa kwenye operesheni usiku na mchana- Makonda

'Watu wanafanya biashara za dawa za kulevya na meli zinazokuja na mafuta'-RC Makonda

'Kuna mama kazi yake ni kusafirisha watoto wa kike ambao wanapewa dawa za kulevya, wawili wako jela China na amewatelekeza'-RC Makonda

'Tukiendelea kuvutanavutana tutapoteza lengo la kupambana na dawa za kulevya'-RC Makonda

'Tukishindwa vita hii ya dawa za kulevya, hajashindwa Makonda au Rais Magufuli tumeshindwa wote'-Rais Makonda

'Tuko na majina 65, nitahitaji kukutana nao ijumaa, wako wanaosemekana wanatumia, wako wanasemekana wanazo taarifa zitakazotusaidia-Makonda

'Nawashukuru wenyeviti wa mitaa wameanza kuleta majina ya watu ambao wanawasiwasi nao kuhusu dawa za kulevya'-RC Malone's

'Kila tunayemuita tunamfahamu kuliko mnavyofikiri kazi yetu ni kuwasikiliza'- RC Makonda

'Zile nyumba mnazozitilia shaka, hamuelewi hata kinachoendelea ni wajibu wetu wananchi kutoa taarifa na taarifa zitakuwa ni siri-RC Makonda

'Kuna ambao tuliwaita wako nje ya DSM, wapo waliotoa taarifa na watafika ila wapo waliokimbia tunawafuatilia na tutawapata wote'- RC Makonda

'Nawashukuru ndugu zangu walioko nchi mbalimbali kwa kunipigia simu na kunipa taarifa mbalimbali'-RC Makonda

Saturday, February 4, 2017

Yabainika: Mjane wa Tanga aliyemlilia Rais Magufuli si tapeli. Nyaraka nyeti zaibuliwa

MJANE kutoka Tanga, Swabaha Mohamed Shosi aliyewashtaki baadhi ya watendaji wa Serikali kwa Rais John Magufuli hapo jana akidai kuzungushwa kupewa haki yake ya mirathi si tapeli kama inavyosambazwa mitandaoni, FikraPevu imejiridhisha.
FikraPevu ililazimika kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba ili kupata ukweli wa tuhuma zilizokuwa zikielekezwa kwa mama huyo mitandaoni na aliithibitishia kuwa Jeshi lake halijawahi kupokea malalamiko yoyote dhidi ya mjane huyo kuhusika na utapeli.
Zimekuwepo jitihada za makusudi mitandaoni zikitoa taarifa zinazoonyesha kuwa kuna watu wanamfahamu kwa undani mjane huyo na kudai ni tapeli aliyekubuhu, bila kuwataja waliowahi kutapeliwa, walitapeliwa nini na lini walifanyiwa utapeli huo.
TUNACHOKIFAHAMU:
FikraPevu imepata kuziona nyaraka mbalimbali zinazohusiana na sakata la mjane huyu ikiwemo barua toka kwa Wakala wa Usajili na Ufilisi (RITA) ya tarehe 13 Februari 2014 kwenda kwa Mkuu wa Upelelezi kuwa nyaraka za ndoa ya mama huyo ni halali.
Aidha, nyaraka nyingine ni mawasiliano kati ya mjane huyo na Wizara ya Sheria na Katiba ikiwemo taarifa iliyoripotiwa Tanga kuhusu mjane kutishiwa maisha yenye RB namba TAN/IR/3371/2012.
Pamoja na hayo, hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Tanga chini ya Jaji P. A. Rugazia ya tarehe 3 Machi 2015 iliamuru mjane huyo asinyimwe haki yake.
KINACHOENDELEA:
Wakulyamba ameieleza FikraPevu kuwa hadi sasa Jeshi lake linayafanyia kazi malalamiko ya mjane huyo na kudai bado hajaiona taarifa inayosambazwa mitandaoni.
“Malalamiko yake mengi ni ya kweli; yapo ambayo tulimshauri aende mahakamani, na yale ya kijinai jeshi linayashughulikia katika hatua mbalimbali” aliongeza Wakulyamba katika mahojiano na FikraPevu.
Kilichotokea jana:
Katika siku ya Sheria duniani, iliyoadhimishwa kitaifa jijini Dar es Salaam jana Februari 2, mjane Swabaha alijitokeza mbele ya Rais Magufuli na kudai kuwa mhimili wa mahakama umeshindwa kumsaidia kupata haki yake ya mirathi na amekuwa akipokea jumbe za vitisho zikiwemo za kutaka kumuua ili asifuatilie mirathi yake.
Kufuatia malalamiko hayo Rais Magufuli aliwaagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP) Ernest Mangu pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) Biswalo Mganga, kuishughulikia kesi hiyo pamoja na kumpa ulinzi ili asidhurike.
Awali Swabaha alimueleza Rais kuwa mtoto wa nje ya ndoa wa marehemu mume wake, Saburia Mohamed Shosi kwa kushirikiana na Wakili wa Mahakama ya Wilaya ya Tanga, Alfred Akaro wameghushi wosia wa mumewe Mohamed Shosi kwa lengo la kumdhulumu mirathi.
Swabaha alidai kuwa, licha ya kushinda katika kesi ya mirathi aliyoifungua mwaka 2010, mahakama ilishindwa kumpa haki yake badala yake wahusika waliishinikiza mahakama hiyo kumfungulia mashitaka mapya saba.
Alisema, suala lake alilifikisha kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Jeshi la Polisi, pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka na kwamba bado halijatafutiwa ufumbuzi.