Wema asomewa mashtaka, aachiwa kwa dhamana
THURSDAY , 9TH FEB , 2017
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu na wenzake wawili wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi ya leo na kusomewa mashitaka matatu yanayohsiana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.
Wema Sepetu akiwa mahakamani leo
Akisomewa mashtaka na wakili wa serikali Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba imeelezwa kuwa msanii huyo alikutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya aina ya bangi kiasi cha gramu 1.08.
Akisoma Shtaka hilo linalowakabili watuhumiwa wote watatu, mbele ya Hakimu Huruma Shaidi wa Mahakama hiyo, Wakili wa Serikali Mtalemwa Kisenyi ameiambia mahakama hiyo kuwa siku ya tarehe 4 mwezi wa pili mwaka 2017 katika eneo la Kunduchi Ununio Jijini Dar es Salaam watuhumiwa hao watatu akiwemo Wema Sepetu walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa ya kulevya kifungu cha 17 (1) (a) cha makosa hayo.
Washtakiwa wote wamekana shitaka hilo, kisha kuachiwa kwa dhamana ya shilingi Milioni 5 na kuwa na wadhamini wawili kila mmoja huku uchunguzi ukiendelea ambapo kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 22 mwezi wa pili mwaka 2017.
Kesi hiyo iko chini ya Hakimu Huruma Shaidi, na mwendesha mashitaka Mtalemwa Kishenyi
0 comments:
Post a Comment