Wednesday, February 15, 2017

Agness Masogange ndani kwa madawa ya kulevya.....stori nzima hii hapa

TAARIFA zilizotufikia, zinaeleza kwamba Video Queen maarufu Tanzania, Agness Gerald almaarufu "Masogange", anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central) akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.

IMG_3342.JPG 

Masogange alikamatwa na Polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba mpaka sasa bado anashikiliwa central.

Mwanadada huyo anaingia kwenye orodha ya wasanii wengine na watu maarufu nchini, walioshikiliwa na wanaoendelea kushikiliwa wakihusishhwa na sakata la matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya, katika vita kali inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Taarifa zaidi kuhusu kukamatwa kwa Masogange zitafuatia...

> Ikumbukwe kuwa tuhuma za Mlimbwende huyu kuhusika na mtandao wa baishara za Dawa za Kulevya zilishawahi kujadiliwa katika uzi huu => Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

sorce jamii forum

0 comments:

Post a Comment