Wednesday, February 8, 2017

RC Makonda atumbua jipu,Nimajina Mapya ya ya wanao jihusisha na Dawa za kulevya jijini Dar es salaam


Kumekucha!!Ni siku nyingine tena,Mkuu wa Mkoa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dsm,ndugu Paul Makonda ataongea leo na waandishi wa habari kuhusu muendelezo wa vita ya madawa ya kulevya ktk jiji la Dsm.

Mkuu wa Mkoa atakuwa mubashara Azam Tv mara ifikapo saa 05:00 asubuhi leo hii.

Tetesi ni kuwa,mkutano huo unaweza kuwa ni kujibu tuhuma za kuwa anawakabili "dagaa" na wakati "mapapa" wa biashara hiyo wapo.Na majibu ya mkuu wa mkoa yatakuwa ni kuwataja hao mapapa na kuelezea hatua zitakazochukuliwa...

Tega usikie....(Stay Tuned)

=======
UPDATE:
=======

Ameanza kwa Kumshukuru Rais wa Jamuhuri.

Paul Makonda asema anataka wauzaji wa dawa za kulevya wajulikane hadharani na hakuna sababu ya kuficha.

Paul Makonda asema vita vya dawa za kulevya vilianza muda mrefu kwa kufutilia hali ilivyo mitaani.

'Kuna watu nilitaka nikutane nao polisi, kuna tofauti kati ya kukamatwa na kuitwa, unapoitwa unapewa nafasi ya kusikilizwa'-RC Makonda


'Kampeni hii dawa ya dawa za kulevya si ya kufanyika kimyakimya tunataka hata watoto wadogo wajue dawa hizi ni hatari kwa afya'-RC Makonda

'Asante kwa watu kama TID, nawapongeza kwa kukiri na kusema kuwa wanatambua namna walivyoingia na kuomba serikali kuwasaidia'-RC Makonda

'Tumemaliza awamu ya kwanza vita ya dawa za kulevya, sasa hii ni awamu ya pili ambayo itakuwa si nyepesi itakuwa na mawimbi mengi-Makonda

'Awamu ya 2 ya vita ya dawa za kulevya tunaianza leo na tunaianza tukiwa tumekamilika, nimekuwa kwenye operesheni usiku na mchana- Makonda

'Watu wanafanya biashara za dawa za kulevya na meli zinazokuja na mafuta'-RC Makonda

'Kuna mama kazi yake ni kusafirisha watoto wa kike ambao wanapewa dawa za kulevya, wawili wako jela China na amewatelekeza'-RC Makonda

'Tukiendelea kuvutanavutana tutapoteza lengo la kupambana na dawa za kulevya'-RC Makonda

'Tukishindwa vita hii ya dawa za kulevya, hajashindwa Makonda au Rais Magufuli tumeshindwa wote'-Rais Makonda

'Tuko na majina 65, nitahitaji kukutana nao ijumaa, wako wanaosemekana wanatumia, wako wanasemekana wanazo taarifa zitakazotusaidia-Makonda

'Nawashukuru wenyeviti wa mitaa wameanza kuleta majina ya watu ambao wanawasiwasi nao kuhusu dawa za kulevya'-RC Malone's

'Kila tunayemuita tunamfahamu kuliko mnavyofikiri kazi yetu ni kuwasikiliza'- RC Makonda

'Zile nyumba mnazozitilia shaka, hamuelewi hata kinachoendelea ni wajibu wetu wananchi kutoa taarifa na taarifa zitakuwa ni siri-RC Makonda

'Kuna ambao tuliwaita wako nje ya DSM, wapo waliotoa taarifa na watafika ila wapo waliokimbia tunawafuatilia na tutawapata wote'- RC Makonda

'Nawashukuru ndugu zangu walioko nchi mbalimbali kwa kunipigia simu na kunipa taarifa mbalimbali'-RC Makonda

0 comments:

Post a Comment