Monday, September 5, 2016

jiwe lililokuwa linazungumza$amaizing speaking rock from Iringa

Kutoka Iringa hili ndilo jiwe linasemekana lilikuwa likizungumza #Gangililonga
13lng
Stori ambazo huwa zinakuwepo mtaani zikihusisha maisha ya eneo fulani hutufanya wengi kuvutiwa na simulizi hizo na kutamani kufahamu hata kidogo undani wa hizo habari zinazosemwa.
Iringa ni mkoa ambao una sifa inayosimamishwa na Mtemi Mkwawa aliyekua chifu na kiongozi mkuu wakati wa upanuzi wa ukoloni wa Ujerumani mwishoni mwa karne ya 19 Iringa.
8lngUkubwa wa jina Gangi lilonga linatokana na Jiwe linalopatikana Manispaa ya Iringa eneo la Gangi Lilonga ambalo kulingana na historia ya eneo hilo na simulizi za jiwe hilo ambalo linasemekana lilikuwa likiongea alikua akilitumia sana Mtemi Mkwawa.
Kwa miaka ya hivi karibuni jiwe hili halitumiki tena kwa imani hizi na kwa sasa limefanywa kama kivutio kwa watalii mbalimbali ambao wanafika kulishangaa,mambo ya Digital kwa sasa wanasema kuwa hakukua na sauti hizo za ajabu.
Kutokana na sehemu yenyewe kuwa mlimani inasemekana kuwa wazee walikua wanashindwa kujua kama ile ni Echo Sound yaani Mwangwi hivyo mtu anaweza kuongea kutoka mbali ukahisi jiwe ndilo linalozungumza.
Tafsiri ya jina hili Gangi Lilonga maana yake  GANGI(jiwe) LILONGA(linaloongea),Mzee Macha ni mwenyeji kidogo Mkoa wa Iringa uwepo wake zaidi ya miaka 30 anashare na sisi anayoyajua kuhusu jiwe hili.
Bonyeza hapa kusikiliza zaidi.
source milladi Ayo

0 comments:

Post a Comment