NDEGE ILIYO AHIDIWA NA RAISI IMEWASILI TANZANIA
Ndege ya kwanza mpya iliyonunuliwa na serikali yawasili jijini Dar-es-salaam
Hii ni ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania -ATCL imewasili jijini DSM ikitokea nchini CANADA ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua mchana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JULIUS NYERERE na kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake.
Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi.
Hii imefuatia ahadi ya Raisi wetu Dr. John Pombe Magufuli ya kuzileta ndege Mpya mbili akiwa madalakani.Ndege hii ni ya kisasa sana na ipo tayali kwa matumizi ya watanzania wote.kuonesha umoja sasa watanzania lazima tujivunie na hiki chetu kwa kusafilia maana sasa shirika limekuja upya na kuahidi huduma Bora kwa watanzania.
0 comments:
Post a Comment