Monday, September 12, 2016

UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO UMEFANIKIWA

WATOTO SITA WAFANYIWA UPASUAJI WA MOYO BURE TANZANIAImage result for muhimbili national hospitalImage result for muhimbili national hospital
Hospitali ya Taifa Muhimbili Taasisi ya Jakaya Kikwete imefanikiwa kuwafanyia upasuaji hadi sasa watoto sita.Haya ni mafanikio Makubwa sana Hapa nchini Ukizingatia kuwa huduma hizi Zinatolewa Bure bila gharama yeyote.Mmoja wa madaktali wanao fanya upasuaji huo alisema "operation ya upasuaji watoto ina changamoto nyingi na operation moja inachukua Mambo mengi,vifaa vingi na matayarisho makubwa,kwahiyo tunaendelea kwa kasi kubwa na tunaendelea vizuli tu".
Image result for muhimbili national hospital
moja ya vifaa muhimu kwa upasuaji
licha ya mafanikio yaliyo fikiwa mpaka sasakatika upasuaji,zoezi hilipia linapata changamoto mbalimbali kama dokta suwende anavyo elezea "changamoto ni nyingi,kuna changamoto zinazo husiana na mgonjwa Mwenyewe,kunachangamoto za hali ya kimazingira kwa maana wazazi,kiuchumi na mahali anapo kaa.ila changamoto ya kiuchumi ndio kubwa kwamaana hakuna mahali hapa nchini vifaa hivi vinapo patikana kwa hiyo vyote tunaagiza kutoka nje.Pia tukisha mfanyia oporation mgonjwa anahitaji damu,dawa na vitu vingine vingi"
Kwa upande wao wazazi walio wapeleka watoto wao kupata huduma hiyo pale Muhimbili wameishukuru serikali na taasisi kwa huduma hiyo kutolewa Bure,kwani wengi wao walikuwa na uwezo mdogo na wasingeweza kumudu gharama za matibabu"Tunamshukuru Mungu kwa kutuletea hii huduma karibu,kwasababu ilikuwa ni gharama sana kwenda India"mmoja wa wazazi alisema
serikali imeweka Mikakati ya kufikia watoto 50-60 ili kusaidia jamii ya watanzania wenye hali ya chini nao waweze kupata Huduma hii.By kihundo

0 comments:

Post a Comment