YOUR WELCOME By ADMIN JERRY KIHUNDO

Let me take this golden chance to welcome everyone around the World,remember that your opinions are very important to us - tanzaniabeautiful.blogspot.com.

M0UNTAIN KILIMANJARO

Kilimanjaro is one of the world's most accessible high summits, a beacon for visitors from around the world. Most climbers reach the crater rim with little more than a walking stick, proper clothing and determination.

MIKUMI

Mikumi National Park abuts the northern border of Africa's biggest game reserve - the Selous – and is transected by the surfaced road between Dar es Salaam and Iringa. It is thus the most accessible part of a 75,000 square kilometre (47,000 square mile)

LET US JOIN TO STOP THIS

No child should be working. Every child has the right to a good education, the right to play and the right to enjoy its childhood. Child labour means that poverty continues to exist. Eradicating child labour means development and better opportunities for everyone.

WE ALL FRIENDS

Everyone is equal in the eyes of God. However people blacks and whites are treated differently in other contries but TANZANIA love and hospitality is our tradition

Wednesday, January 17, 2018

Sisi Hatujakataza uvaaji wowote wa nguo-Lazaro Mambosasa

‘Hili suala la Kuzuia vimini na viduku limezushwa, Mimi niliitisha Press kuelezea mafanikio ya Jeshi la Polisi Kwa kanda maalum Kwa kipindi hiki cha sikukuu kilichopita.
.
Na hili swali niliulizwa nikasema kuwa linavunja maadili na huu si utaratibu wetu ni watu wa magharibi si maadili yetu kabisa lakini kwetu bado sio kosa kisheria.’ - Kamanda wa Polisi Dar Lazaro Mambosasa akifafanunua kuhusu taarifa ya kukataza watu kuvaa nguo fupi on Power Breakfast-CloudsFm

Monday, January 15, 2018

CHIRWA AFUNGIWA MECHI TATU

Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa amefungiwa kucheza mechi tatu za ligi kuu Tanzania Bara na kutozwa faini ya shilingi laki tano kwa kosa la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyokutana Jumapili Januari 14, 2018 na kusikiliza kesi hiyo iliyowasilishwa na Bodi ya Ligi ikihusu mchezo namba 83 kati ya Yanga na Tanzania Prisons iliyochezwa Novemba 25, 2017 kwenye Uwanja wa Azam Complex Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, Chirwa alifika kusikiliza kesi hiyo akiwa na muwakilishi wake na alikiri kutenda kosa hilo.

“Kamati baada ya kumsikiliza Chirwa na kupitia video za mchezo huo pamoja na taarifa ya kamishna  na muamuzi imetoa adhabu kwa mchezaji huyo kupitia kanuni ya 37(7b) na kanuni za nidhamu za TFF kifungu cha 48(1d) na 48(2)”. Imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
@tanzania.beauty

Saturday, January 13, 2018

Rais wa Rwanda Amesha tua uwanja wa ndege wa JK

Rais wa Rwanda, Paul Kagame amewasili Uwanja wa ndege Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja nchini.

Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa taarifa zaidi.

@tanzania.beauty #tanzaniaBeauty #tzbeauty

Friday, January 12, 2018

LEO KATIKA HISTORIA:

Mwaka1964: Wazanzibari wapigania Uhuru waliipindua Serikali ya Sultan Jamshid bin Abullah na kuanzisha utawala wao huru chini ya Abeid Amani Karume. Miezi mitatu baadaye Zanzibar iliungana na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Thursday, January 11, 2018

Miaka 54 Ya Mapinduzi Ya Zanzibar

Leo ni siku muhimu sana kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo wanakumbuka namna walivyoweza kupindua utawala wa Kikoloni kutoka kwa Sultan ambapo kwenye utawala huo hakukuwa na haki na usawa kwa Wazanzibar, ukweli utabaki palepale kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yana thamani kubwa sana katika maisha ya wakazi wa Visiwani humo.

Mzee Omar Msongoro, mmoja wa waliokuwa wapiganaji mstari wa mbele ili kufanikisha Mapinduzi Matakatifu amesema kuwa siku hiyo January 12 mwaka 1964 wakati Mapinduzi hayo yanatokea tayari kulikuwa kuna maandalizi yaliyokwisha andaliwa kupitia kanda tofauti za Visiwani humo....
Tanzania Beauty 🚩 🚩 🚩

Sunday, January 7, 2018

Lissu afika salama Ubelgiji

Na, Saed Kubenea

MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amewasili salama nchini Ubegiji alikokwenda kwa matibabu.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa maofisa wa serikali nchini humo zinasema, Lissu aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Zaventem, majira ya saa 11:40 ya jioni ya jana Jumamosi.

Lissu aliingia nchini humo kwa ndege ya shirika la ndege la Uholanzi (KLM), ambayo ilimchukua kutokea Amsadam, Uholanzi.

Mwanasiasa huyo machachari wa upinzani nchini, alianza safari yake ya matibabu ya tatu kutokea Nairobi, Kenya.

Aliondoka nchini Kenya kwa ndege ya shirika la ndege la nchi hiyo KQ, saa mbili asubuhi ya  Jumamosi.

Kwa mujibu wa afisa huyo wa serikali nchini Ubegiji, Lissu alipokelewa uwanja wa ndege chini ya ulinzi mkali wa maofisa wa polisi na wale wa usalama.

Aidha, ulinzi umeimarishwa pia kwenye hospitali (jina tunalihifadhi kwa sasa), aliyopelekwa kwa matibabu.

Lissu alishambuliwa kwa risasi, Septemba mwaka jana akiwa nyumbani kwake Area D, mkoani Dodoma. Alikuwa akitokea bungeni alikokuwa anahudhuria mkutano wa Bunge.

Breaking news.. Simba coach yachomwa saa hii kijiwetanga baada kugonga jamaa wa pikipiki na kumuua.. Kaa nasi kwa habari kamili

Simba coach yachomwa saa hii kijiwetanga baada kugonga jamaa wa pikipiki na kumuua..

Kaa nasi kwa habari kamili

Saturday, January 6, 2018

Rais Magufuli atia hodi mwaisela kumjulia hali Kingunge. Soma zaidi>>>

Rais Magufuli amjulia hali Mzee Kingunge Ngomable Mwiru aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela, hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Mzee Kingunge amelazwa hospitalini hapo akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.

Hali ya Mzee Kingunge inaendelea vizuri

Instagram @tanzania.beauty

Facebook : Tanzania Beauty 🚩

Tweeter : @tanzaniabeauty

Tundu Lissu anaelekea Ubelgiji kwa matibabu zaidi

‪NAIROBI, KENYA: Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu(CHADEMA) leo Saa 2.30 asubuhi anaondoka jijini Nairobi kwenda Ubelgiji kwa matibabu zaidi

- Lissu anaendelea na matibabu kufuatia shambulizi lililofanyika dhidi yake huko Dodoma na kupigwa risasi 16 huku 8 zikimwingia mwilini na 7 zimeshatolewa na madaktari wa Dodoma na Nairobi

Tanzania Beauty 🚩🚩🚩

Mapindi Cup 2018

MSIMAMO: Kabla taifa halijashuhudia mchezo mkali katika michuano ya #MapinduziCup2018 utakaowakutanisha mabingwa watetezi Azam FC dhidi ya mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Simba SC saa 2:15 usiku wa leo, msimamo katika makundi yote umekaa hivi....

Kwa msimamo huu, Azam ikifungwa leo, inakuwa imeaga mashindano kwa kuwa huu ndiyo mchezo wake wa mwisho, lakini Simba bado itakuwa na mchezo mmoja, hivyo ikifungwa leo, itabidi kusubiri matokeo yake ya mchezo wa mwisho.

Fuatilia michuano hii kupitia Facebook page yetu ya hapa itakupa majibu mbashara kutoka dimba la Amaan Zanzibar. na instragram page yetu ya @tanzania.beauty